Surprise Me

Serikali Kuyaboresha Mashindano ya Golf, Utalii Karibu Kusini - HDMaza.pw

Jul 30, 2018 2 1 676

Serikali Kuyaboresha Mashindano ya Golf, Utalii Karibu Kusini...... IRINGA: JULAI 29, 2018; WAKATI mashindano ya golf ya Utalii Karibu Kusini Mufindi Golf Challenge 2018 yakihitimishwa leo kwenye Viwanja vya Golf vya Unilever wilayani Mufindi, serikali imeahidi kuendelea kuyaboresha mashindano hayo ili yatumike kwa ufanisi zaidi kutangaza vivutio vya Utalii katika kanda za Nyanda za Juu Kusini. Akizungumza kwenye viwanja hivyo, Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Utalii Wizara ya Mali Asili na Utalii, Bw Deogratius Mdamu alisema uamuzi wa Serikali kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa kutumia mashindano hayo kutangaza Utalii wa Nyanda za Juu Kusini umeonesha mafanikio licha ya kuwa mashindano hayo yanafanyika mara ya kwanza baada ya kupita miongo kadhaa... Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mashindano hayo wamesema uwepo wa mashindano hayo utatumika kikamilifu kutangaza fursa na vivutio vya Utalii vinavyopatikana katika ukanda huo. Bw Yeckonia Chaula ambaye ni mchezaji mwandamizi wa golf kutoka klabu ya Golf ya Mufindi alisema: Naye Mratibu wa Mashindano hayo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI) Bw Clement Mshana aliwashukuru sana washiriki hao hususani klabu ya Golf ya Lugalo kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mashindano hayo huku akiahidi kutumia maoni ya washiriki katika kuboresha zaidi mashindano hayo mwakani. Mashindano hayo ya siku tatu yalihusisha washiriki zaidi ya 80 wakiwemo wachezaji wa kulipwa yaani ‘Professionals’ na washiriki wa kawaida yaani ‘Amateurs’ na yanatarajiwa kuhitimishwa leo ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Tamisemi, Bw Joseph Kakunda. Install GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Suazi1 http://www.youtube.com /c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari INSTAGRAM: https://www.instagram.com/globalpubli..Tags: mashindano ya golf    kuboresha utalii kusini    global tv online    
eXTReMe Tracker
HDMaza.pw